Anthonio


Breaking News

About

Become a Fan

Monday, 21 July 2014

SANDRA: NAIPENDA SANA NDOA YANGU

TAHADHARI
Mimi nakukubali sana Sandra, kwanza nakupa hongera kwa kazi zako nzuri, ila nakupa tahadhari, jitahidi hivyohivyo kuwa na msimamo wa kutopata skendo, vinginevyo utajiharibia katika sanaa pia jamaa atakumwaga kwani utapoteza sifa. Selemani Alifa, Dar, 0718803204
SANDRA: Asante, nitajitahidi.

Staa wa filamu Bongo, Salma Salmini 'Sandra'.
UCHUMBA
Sandra nakuzimia sana jinsi ulivyo na umbo zuri, naomba uwe mchumba wangu wa kuniliwaza kimapenzi. Salim Liundi, Dar, 0659601205
SANDRA: Utanisamehe, nimeshaolewa, siwezi kuwa tena mpenzi wako.

MAFANIKIO
Nakukubali sana Sandra ila nataka kujua ni mafanikio gani uliyoyapata kutokana na tasnia hii ya uigizaji? Amiri Salumu, Dar, 0653252416
SANDRA: Mafanikio nimepata mengi sana kubwa zaidi nimeweza kufahamiana na watu wengi. Nimepata mume kupitia sanaa na mengine mengi ambayo siwezi kuyataja kwa sasa ila mashabiki wangu watayaona.

ELIMU YA SANAA
Dada Sandra bila shaka kipaji unacho lakini je, kuhusu elimu ya sanaa unajiendeleza au unategemea kipaji tu? Rama Nuru, Dar, 0682885844
SANDRA: Napenda sana kujiendeleza kielimu lakini bado sijapata fursa zaidi ila nimesoma kozi fupifupi za sanaa.

Salma Salmini 'Sandra' akipozi.
SWALI
Hivi mumeo bado uko naye na mna watoto wangapi? Vipi mumeo anapendezwa na kazi yako ya sanaa? Muddy Madley, 0652672805
SANDRA: Mume wangu nipo naye, tuna watoto wawili na mume wangu anapendezwa na kazi yangu kwa sababu alinikuta kwenye sanaa.

HISTORIA
Mimi ningependa kujua historia yako kwa ufupi. Neema, Dar, 0717579055
SANDARA: Nimezaliwa Shinyanga, nina elimu ya kidato cha nne pia nimesomea usekretari katika Chuo cha Magogoni, Dar. Nilianza sanaa mwaka 2002 katika Kundi la Kaole.

NDOA
Dada Salma mimi napenda sana kazi yako ila nakushauri kuichunga na kuilinda ndoa yako kwani heshima ya mwanamke ni ndoa, Mungu akujalie upeo zaidi. Emmanuel George, 0765171432
SANDRA: Asante nami naipenda sana ndoa yangu jamani na ninamuomba Mungu anisaidie.

NI KWELI SANAA IMESHUKA?
Kwa mtazamo wangu sanaa yenu imeshuka kutokana na kuendekeza uhuni, je, wewe kama mkongwe unaionaje? Prince Dulla, 0652749414

SANDRA: Siwezi kujua kwa sababu kila mtu ana malengo yake yaliyomfanya aingie kwenye sanaa. Wasanii walioanzia kwenye vikundi wanajua thamani ya sanaa ndiyo maana wanajiheshimu lakini wale ambao hawakupita kwenye vikundi wengi ndiyo wana tabia hizo. Mimi naipenda sana sanaa na ni kazi yangu ninayoiheshimu.
BIFU NA BATULI VIPI?
Pole na majukumu dada Sandra, hivi lile bifu lako na Batuli bado hamjalipatia ufumbuzi? Yaongeeni myamalize ili muwe kitu kimoja. Said, Dar, 0718000790
SANDRA: Sina bifu na Batuli wala msanii yeyote maana maisha yenyewe mafupi haya, mimi na Davina tuligombana lakini tulishayamaliza.

ETI HAKULIPWA NA DUDU BAYA?
Sandra eti ni kweli hukulipwa na Dudu Baya kwenye ile video ya Nakupenda Mpenzi? Manuely Cimmario, Tanga, 0652153571
SANDRA: Alinilipa hela ya kawaida siyo nyingi.

UKIMYA
Sandra wewe ni mmoja wa wasanii wakali sana wa maigizo kwenye runinga enzi hizo na akina Kanumba, imekuwaje jina lipotezwe na watoto, nini shida? Noel Kibere, Moshi, 0714300280
SANDRA: Jina langu halijapotea bado lipo, unajua niliolewa baada ya hapo nikawa nalea nilivyorudi nikawakuta wasanii hao wapya na hawajaolewa ndiyo maana wanawika kutokana na kwamba hawana majukumu.

ANAZIKWEPA VIPI SKENDO?
Kwanza napenda kukupongeza dada Sandra kwa kazi nzuri, pili nataka kukuuliza unawezaje kuepuka skendo wewe kama mtoto wa kike? Amisa, Dar, 0655603091
SANDRA: Ni kujiheshimu tu.

HUYU ANAMJUA SANA
Nakufahamu Salma, ulikuwa unasoma Alharamain Secondary na rafiki yako mkubwa alikuwa ni Amina mdogo wake MwanaFA (Hamis Mwinjuma), vipi unakumbuka viboko vya Ustadh Abdallah? Mrs Thomas, Dar, 0719353468

SANDRA: Yote ni kweli na hivyo viboko navikumbuka sana.
Read more ...

SHETTA AMWAGIWA UJI WA MOTO

KHA! Staa wa Kerewa, Nurdin Bilal ‘Shetta’ juzikati alijikuta katika wakati mgumu baada ya kumwagiwa uji wa moto na Mbongo-Fleva mwenzake, Mwajuma Abdul ‘Queen  Darleen’.
Staa wa Kerewa, Nurdin Bilal ‘Shetta’ akipewa dozi ya maji.
Tukio hilo la aina yake lilijiri muda mchache baada ya tafrija iliyoandaliwa na uongozi wa No Fake Zone ‘NFZ’ kwa ajili ya uzinduzi wa video mpya ya Linah na kuaga rasmi menejimenti ya Jumba la Vipaji Tanzania (THT) pande za Kinondoni jijini Dar.
‘Shetta’ aliyelowa chapa chapa.
“Unajua leo ni siku ya kuzaliwa ya Shetta, ikiisha tu hii shughuli namuita nje na kummwagia maji yeye mwenyewe anajua sisi hatujui,” alisikika Ommy Dimpoz.
Linah Sanga akizungumza jambo katika tafrija iliyoandaliwa na uongozi wa No Fake Zone ‘NFZ’ kwa ajili ya uzinduzi wa video yake mpya.
Baada ya tukio hilo ndipo Shetta alipotoka nje na kukutana na ishu hiyo ya kummwagia maji kisha Queen Darleen akamaliza mchezo kwa kummwagia uji.
Read more ...

KAJALA: PERFECT SIO MPENZI WANGU

Acha bwana! Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’ ameibuka na kukanusha vikali madai ya kutoka kimalovee na mtangazaji wa Clouds aitwaye Perfect.
Staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita jijini Dar, Kajala alifunguka kwamba madai hayo hayana ukweli wowote na wala hana ukaribu na mtangazaji huyo.
Mtangazaji wa Clouds aitwaye Perfect.
“Sina relation (uhusiano) kama huo na Perfect zaidi ya kazi tu,” alisema Kajala huku Perfect akiwa hapatikani hewani kila alipotafutwa.
Read more ...
Designed By